top of page
  • Writer's pictureOrina Ontiri

TAARIFA YA HABARI 06/04/2015

 — karibu kwa taarifa zetu jioni/asubuhi hii  wakati wa kupokea habari za yard na AGR fm lakini kwanza tupate mkhutasari wake –Ni maisha yetu lazima tume ya TSC itujali maslahi  yetu walimu wa –masaba kazikazini wasimama kidete. –Msipofanya kazi vizuri zitawapatia pesa mwakilishi wa magenche awambia wanakandarasi –Kanisa zote zaombwa kushirikiana kupambana na madawa za kulevya kisii hujambo

1 Walimu kutoka wilaya ya Masaba kaskazni wameiomba tume ya kuwaajiri  walimu [TSC] kuwajali  wakati wa kuwahamisha  walimu hao hadi shule zingine. Akiongea hiyo jana katika  eneo la  Masaba kaskazini kaunti ya Nyamira  mwenyekiti wa walimu kutoka masaba Meshack Obonyo ameiomba tume ya kuwaajiri walimu [TSC] kuzingatia afya na masuala mengine ya walimu kabla ya kuwahamisha  hadi shule  zingine. Kulingana na Meshack walimu uhamishwa kuenda katika shule zingine ambazo ni mbali kutoka  sehemu wanakoishi   jambo ambalo amesema huwa ngumu kwa walimu hao kwani  kiwango cha pesa wananachokabidhiwa  cha maruburubu ni kidogo mno ambacho hakiwatoshi katika  shughuli zao za kila siku.. Huku  Mwekahazina   Evans Karuru akiomba tume hiyo kuzingatia afya ya walimu  kabla ya kuwahamisha hadi  katika shule zingine. 2 Mwakilishi wa wadi ya Magenche iliyoko eneo bunge la Bomachoge Borabu Kaunti ya Kisii Timothy Ogugu ametishia kurudisha pesa za maendeleo za wadi yake kwa serikali ya kaunti baada ya mwanakandarasi aliyepewa kandarasi ya kujenga zahanati ya Kiabugesi kualibu ujenzi huo na kusema jinsi mwanakandarasi huyo alijenga si halali. Akizungumza jana katika wadi yake mwakilishi huyo alishangazwa jinsi mwanakandarasi huyo alifanya ujensi wa zahanati hiyo ya Kiabugesi ilyoko wadi yake na kusema atazirudisha pesa hizo kwa serikali ya kaunti au kuanzisha ujenzi huo upya  baada ya kuthibitisha kuwa mwanakandarasi huyo hualibu kazi na kusema hakuna haja ya kukabidhiwa pesa hizo. Aidha, mwakilishi huyo aliwaonya wanakandarasi wote katika wadi yake ambao hawafanyi kazi kunavyostahili kuchukuliwa hatua ya kisheria kwani pesa zinazotumika ni za mkenya wa kawaida kufanyiwa maendeleo. . Mwakilishi huyo alianzisha ujenzi wa zahanati 6 katika wadi yake hiyo jana kwa kutumia pesa hizo za maendeleo huku akiwaonya wanakandarasi kuwa wakialibu ujenzi huo basi hawatapokezwa pesa ila kurudisha kwa serikali pesa hizo au kuanza ujenzi huo upya Miongoni mwa zahanati alizoanzisha hiyo jana ni Eberege ,Nyabiore,Itembu,Riogachi na Magenche na wakati huo pia alianzisha ujenzi wa madarasa ya ECD katika shule za msingi katika wadi hiyo

3 Baada ya ahadi nyingi za kuboresha huduma za afya katika kaunti ya Kisii, gavana wa Kaunti hiyo James Ongwae mwishowe ametia saini ya ufadhili wa kujengwa kwa kituo cha saratani katika hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii. Ufadhili huo wa zaidi ya shilingi bilioni 2, fedha hizo zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika(BADEA), kulishuhudia gavana Ongwae, Henry Rotich waziri wa Fedha  na mkurugenzi mkuu wa benki hiyo ya BADEA Bwa Yousef Ibrahim Al Bassam, Gavana huyo wa Kisii akipokezwa hundi ya hela hizo huko jijini Nairobi. Akiongea na waandishi wa habari baada ya kutia saini mradi huo jijini Nairobi, Bwa Ongwae alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho utaanza kabla ya mwisho wa mwaka huu ambapo alimshukuru mkurugenzi mkuu wa benki hiyo ya BADEA kwa kufadhili mradi huo wa ujenzi wa kituo ulikuwa mojawapo ya ahadi alizotoa gavana huyo katika harakati za kuboresha na kuimarisha huduma za afya kwa wagonjwa na wale wanaotembelea hospitali ya Kisii .

4 Kasisi wa kanisa ya katholiki katika chuo kikuu cha Kisii Lawrence Nyaanga ameomba kanisa zote kushirikiana na kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya katika jamii. Akiongea jana, Jumatano katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kisii wakati shirika la Kupambana na madawa ya kulevya nchini NACADA lilipoanzisha mafunzo na fahamisho juu ya hatari ya madawa za kulevya, Nyaanga aliomba kanisa zote kushirikiana kwa pamoja ili kufunza wakaazi kuhusiana na madhara ya madawa hayo Shirika la kupambana na madawa ya kulevya, NACADA, likishirikiana na chuo kikuu cha Kisii walianzisha kampeini ya siku tatu mfululizo huku siku ya ijumaa itakuwa ni kupita katika barabara za mji wa Kisii ili kuwafahamisha na kuwaelimisha wakazi juu ya hatari ya madawa ya kulevya, huku mwenyekiti wa shirika hilo John Mututho akitarajiwa kuhudhuria hafla hiyo. Imeandaliwa na Denis zadock mwanahabari wetu ,Peter Onkoba Producer, Brighton Makori Reporter @  yard fm na AGR FM 4th juni  2015

Global Radio Network

0 views0 comments
bottom of page