Yaliyotukia Hii Leo Kwa Ufupi...1. Washukiwa 7 wamekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo cha Sayansi na Kilimo cha Jomo Kenyatta. Inaripotiwa kwamba Joel Juma alidungwa kisu mara kadhaa tumboni na kifuani na watu wasiojilikana akiwa na mpenziwe Jumanne asubuhi. Wanafunzi wameandamana hadi kwenye kituo cha polisi cha Juja wakitaka genge la wahalifu linalowavamia na kuwatishia kukabiliwa na polisi.


2. Kukabidhiwa kwa tikiti ya Jubilee kwa aliyekuwa naibu gavana wa Nairobi Polycarp Igathe kugombea kiti cha ugavana Nairobi kumezua hisia kali kutoka kwa wafuasi wa wagombea Agnes Kagure wale wa mwanabiashara Richard Ngatia, ambao wamekuwa wakitarajia kupewa tikiti hiyo. Baadhi ya wafuasi wamekashifu hatua hiyo huku wakisema kwamba Igathe alijiondoa afisini alipokuwa naibu wa gavana, wakiongeaza kwanba hawatambui utendakazi wake.


3. Rais Uhuru Kenyatta ameelezea ufanisi wa serikali yake katika kuinua sekata ya elimu nchini. Akizungumza kwenye kongamano la 45 la walimu wakuu wa shule za sekondari huko Mombasa, Rais amepongeza washikadau wanaoshirikiana kufanikisha mtaala mpya wa elimu wa CBC kwa kile anasema ni sehemu muhimu inayowaandaa wanafunzi kukabiliana na maisha ya baadaye. Akizungumza katika kongamano hilo, waziri wa elimu Profesa George Magoha amempongeza rais kwa kufanikisha uajiri wa walimu zaidi ya 120,000.11 views0 comments