top of page
  • Writer's pictureOrina Ontiri

YANAYOJIRI 06/06/2015


–Ni wakati wa kupokea habari za yard fm lakini kwanza tupate mkhutasari wake.

—Ni haki yetu kutengenezewa barabara wakaazi wa Nyaribari Masaba wasimama kidete

—-Lazima gavana atueleze yale ametekeleza kimaendeleo kwa kaunti ya Nyamira mbunge wa Kitutu Masaba Timoty Bosire akariri

—-Soko la Gesusu kupata sura mpya karibuni

—Wanahabari wa Kisii wajipata matatani tena kwa kutoa habari si halisi

1   wakaazi wa eneo Bunge la Nyaribari Masaba, Kaunti ya Kisii waliandamana hiyo jana, kulalamikia  hali mbaya ya barabara ya kutoka makutano ya  Geteri  kuelekea soko la Geteri ambayo kwa sasa haipitiki.

Waendeshaji Bodaboda waliojawa na gadhabu walilalamikia hali duni ya barabara hiyo ambayo kwa sasa haipitiki kamwe kufuatia mvua nyingi inaendelea kunyesha katika sehemu za Kisii.

Vijana hao wakiongozwa na mwenyekiti wa Bodaboda wa eneo hilo Mong’eri Nyabicha walichukua hatua ya kupanda mgomba wa ndizi katika barabara hiyo na kutatiza usafiri wakidai kwamba kuliilima barabara hiyo ili suluhisho ipatikane kwani wanaofaa kushughulikia ukarabati wa barabara hiyo wamekosa kuwajibika.

Wakiimba wimbo wa haki yao, vijana hao wamemtaka Mbunge wa eneo hilo Elijah Moindi kuikarabati barabara hiyo ambayo inaunganisha Kaunti ya Kisii na ile ya Narok.

Waakazi wengi kutoka eneo hilo wakiwa wakulima na kutegemea barabara hiyo kwa kusafirisha mazao yao kuenda sokoni sasa wamesema biashara yao imeathirika.

2  Mbunge wa eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira Timothy Bosire ametishia kuongoza maandamano kulalamikia uongonzi mbaya wa kaunti ya Nyamira

Akizungumza jana  katika uwanja wa shule ya msingi ya Rikenye iliyoko wadi ya Rigoma kaunti ya Nyamira wakati alikuwa anaikabidhi shule hiyo pesa za ustawi maeneo bunge CDF,  mbunge huyo alisema huenda aongonze maandamano kulalamikia uongonzi mbaya wa kaunti ya Nyamira.

Aidha mbunge huyo alisema tangu serikali za kaunti kuanzishwa kwa miaka mitatu iliyopita serikali ya kaunti ya Nyamira ndio imerudi nyuma kimaendeleo  huku akitoa mfano wa kaunti ya Kisii ambayo inaongozwa na gavana James Ongwae akisema Ongwae amefanya maendeleo zaidi kuliko kaunti ya Nyamira

Naibu gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi amesema madawa ya kulevya ni changamoto kubwa kwa jamii  ya mkisii na kusema utumiaji wa madawa hayo unastahili kuangaliwa zaidi kama magonjwa mengine .

Akiongea na waadishi wa habari hii  leo afisini mwake iliyoko mjini Kisii  naibu huyo  Maangi alishukuru kampeini ya kupambana na madawa ya kulevya ambayo imefanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha Kisii kwa siku tatu mfululizo huku chuo hicho kikishirikiana na tume ya kupambana na madawa ya kulevya  nchini  NACCADA na kusema hiyo ndio njia moja ya kupunguza kuvunjwa kwa sheria hapa nchini

Wakati uo huo ,aliomba vyombo vya habari kuelimisha wakenya hadhari za kutumia madawa ya kulevya kila siku kama njia mojawapo ya kupunguza  utumiaji wa madawa hayo katika jamii.

4 Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nyamira Alice Nyachoka Nyachoka Chae amesema baadhi ya viongonzi kutoka kaunti hiyo wamejaribu kushirikiana na Gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama kufanya maendeleo lakini  juhudi zao zimegonga mwamba.

Akiongea hiyo jana katika mji wa Nyamira mwakilishi huyo alisema uongonzi uliopo kwa kaunti ya Nyamira  si halali.

Inasemekana kuwa gavana wa kaunti hiyo hana maendeleo kamwe  na hataki kushirikiana na viongonzi wa kaunti hiyo jambo ambalo limewalazimisha viongonzi  wa eneo hilo kukosoa uongonzi wa gavana huyu

Aidha mwakilishi huyo amewataka viongonzi wote akiwemo gavana wa kaunti hiyo  John Nyagarama ,wabunge ,wawakilishi wa wadi  seneta pamoja naye mwakilishi wa wanawake kushirikiana ili kuleta maendeleo katika kaunti ya nyamira kwani kaunti hiyo iliorodheshwa kuwa miongoni mwa kaunti zilizofanya vibaya zaidi kwa maendeleo.

5 Shule ya Msingi ya Riomanga iliyoko wilayani Masaba kaskazini eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira ilifadhiliwa na talakilishi kutoka kwa afisa mkuu wa benki ya dunia Charles  Mochama.

Akizungumza   jana katika uga wa shule hiyo ya Riomanga afisa huyo mkuu wa benki ya dunia Charles Mochama alisema  ameanzisha mradi wa kufadhili shule za msingi ambazo ziko kwa zone ya Bochari talakilishi kama njia moja ya kuinua viwango vya elimu  katika eneo hilo.

Aidha, afisa huyo alisema talakilishi hizo zitasaidia shule hasa walimu kutengeneza makaratasi ya maswali ya mitihani hali maarufu examination question papers] ili wanafunzi wawe wakifanyishwa mitihani baada ya kila mwenzi badala ya kutumia pesa nyingi kununua mitihani,

Hafla hiyo ilihudhuliwa na mwenyekiti wa chama cha KNUT katika wilaya ya Masaba kaskazini Meshack Obonyo.

6  Wakaazi wa Wadi ya Gesusu eneo bunge la Nyaribari Masaba kaunti ya Kisii wameombwa na mwakilishi wa wadi hiyo Sammy Keronche kushirikiana ili kuimarisha viwango vya maendeleo katika eneo hilo.

Akizungumza jana  ofisini mwake Keronche aliwataka wakaazi wa wadi hiyo kushirikiana wakati wa kuweka mikakati ya maendeleo ili wawe na lengo moja kimaendeleo kama wadi.

Wananchi wa wadi hiyo sasa wana la kutabasamu kwani soko mpya la gesusu  limejengwa ambalo litafunguliwa hivi karibuni katika eneo hilo.

7 Licha ya mfungwa mmoja kumshambulia afisaa wa gereza kuu la Kisii, naibu afisaa mkuu msimamizi wa gereza hilo Benjamin Boit,   amejitolea kuimarisha na kuboresha uhusiano ulioko baina ya wafungwa na wanausalama wa gereza hilo.

Naibu huyo alisisitiza kuwa bado mna mwelekeo na uhusiano dhabiti miongoni mwa wafungwa na mafisaa wa kituo hicho.

Akithibisha kisa cha wiki jana ambapo afisa wa gereza hilo alishambuliwa na mfungwa kwa kijembe na kukatwa kwenye pua na kuchanwa kwenye kipaji cha uso,

 Boit alisema kuwa afisa huyo alikuwa katika shughuli ya kawaida kukagua wafungwa ambapo mmoja wa wafungwa alichomoa kifaa chenye makali na kumjeruhi.

Hata hivyo, Boit alifafanua kuwa afisa huyo alishapata matibabu na anaendelea vizuri kiafya, huku akisema kuwa mshukiwa ambaye amewahi kufungwa kwenye gereza hilo hapo awali atachukuliwa hatua ya kisheria kwa kitendo hicho.

Naibu msimamizi huyo aliwataka wanahabari kuwajibika kwa kutoa ripoti halisi kunapotokea shida, ambapo alishangaa zile habari ziliandikwa kuhusiana na kisa hicho zikidai kuwa afisa aliumiza mfungwa.

Prepared by Denis zadock news anchor yard fm 6 th june 2015

Global Radio Network

6 views0 comments

Comments


bottom of page